MWAMUZI pekee wa
Tanzania ambaye amewahi kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia za Vijana, Hafidh
Ally amefariki dunia jana, usiku katika hospitali ya General
Dodoma alikopelekwa kwa matibabu.
Hafidh Ally alichezesha fainali za Vijana U-16 zilizofanyika nchini
Scotland mwaka 1989 na alikuwa mwamuzi
pekee kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambaye amewahi kuchezesha fainali
za mataifa huru ya Afrika (CAN) (kwa sasa AFCON) kwa miaka sita mfululizo
Fainali za Mataifa Huru Afrika ambazo hufanyika kila baada ya miaka
miwili, Hafidh alichezesha ni 1984 hadi
zile za mwaka 1994 ambapo 1984 ndio alikuwa bingwa
Cameroon, 1986 Misri ikaibuka bingwa, 1988 akawa bing
waCameroon
1990 wakawa bingwa Algeria, 1992 bingwa ni Ivory Coast na 1994 akachukua ubingwa Nigeria
Akizungumza na gazeti hili mmoja wa waamuzi wastafu, Lesley Liunda
ambaye pia ni kamishna na mkufunzi wa CAF, alisema Tanzania imepoteza moja ya
alama muhimu kwenye tasnia ya uamuzi ambayo haijawahi kufikiwa na yeyote.
"Mimi nilimkuta Hafidh kwenye uamuzi, alinipokea vizuri na alikuwa
ni mtu muwazi na aliyependa kusaidia wenzake nasikitika ameondoka wakati bado
mchango wake unahitajika", alisema Liunda.
Pia Liunda alisema kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati hakuna mwamuzi
aliyeweza kuvunja rekodi ya Hafidh Ally ya kuchezesha Mataifa Afrika kwa
mfufulizo mara sita.
"Kwa Afrika unaweza kupata waamuzi ambao hawazidi watatu
waliochezesha mataifa kama Hafidh kwa mfufulizo hata akina Masembe wa Uganda
hawajamfikia", alisema Liunda.
Liunda ambaye alikuwa mwamuzi msaidizi wa FIFA alisema amewahi
kuchezesha na Hafidh mechi za Simba na Yanga na kwenye Ligi ya Muungano na
kudai kuchezesha naye unafurahia.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Selestine
Mwesigwa alisema shirikisho limepokea kwa masikitiko kifo chake kwani TFF wamepoteza
mtu muhimu kwenye soka la Tanzania
“Jina
la Hafidh ni linabeba dhana zima ya waamuzi Tanzania na Afrika kwani alikuwa mkufunzi
na kamishina ambaye anatambuliwa na CAF na FIFA hivyo kuondoka kwake ni pengo
kwetu TFF kwani tumepoteza mtu muhimu", alisema Mwesigwa .
Hafidh pia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi, (CCM),
Pamoja na wasifu huo Hafidh alikuwa mpenzi na mwanachama wa klabu ya
Yanga na juzi alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tawi la Yanga Bungeni Dodoma
chini ya mwenyekiti Venance Mwamoto, na Makamu Ridhiwani Kikwete.
Hafidh alizaliwa Oktoba 30, mwaka 1953 visiwani Zanzibar na aliwahi kuwa
Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005
hadi mauti yanamkuta.
No comments:
Post a Comment