Vituo
vya Utamaduni wa China zaidi ya 20 katika nchi tofauti duniani
vitafanya maonyesho ya utamaduni wa nchi hiyo pamoja na kuenzi wasanii
waliohamasisha jamii ya wachina kuenzi tamaduni zao.
Mshauri
wa Ubalozi wa Watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania, Gao Wei amesema
kwa hapa nchini maonyesho hayo yatafanyika kuanzia Novemba 12 hadi 24,
2016 katika kituo cha utamaduni wa China kilichopo Upanga, jijini Dar es
Salaam.
“Mwaka
huu tunafanya maonyesho na kumbukumbu ya mwandishi wa tamthilia za
China William Shakespeare na msaidizi wake Tang Xianzu, kutokana na
mchango wao katika ulimwengu wa Tamthiliya. Kumbukumbu hii itafanyika
katika vituo vya kitamaduni za China vipatavyo 26 katika nchi
tofautitofauti,” amesema na kuongeza.
“Maonyeshi
hayo pia yanafanishwa na maisha na kazi za wasanii hao ambao
walihamasisha jamii ya China kudumu na kuenzi tamaduni zao.”
Amesema maonyesho hayo yataambatana na burudani ya muziki wa asili ya China na mashairi.
“Maonyesho hayo pia yatawezesha wageni kuelewa tofauti ya tamaduni za nchi za mashariki na magharibi,” amesema.
No comments:
Post a Comment