Mashabiki
42,123 ndiyo waliingia uwanjani kwa kulipa katika mechi ya Jumamosi kati ya
Yanga dhidi ya watani wake Simba.
Mechi hiyo
iliyoisha kwa sare ya bao 1-1, Jumla ya Sh milioni 357 zilipatikana kwa mujibu
wa kampuni ya Selcom.
Meneja
Miradi wa Selcom, Gallus Runyeta amesema hayo ni mapato yaliyopatikana kutumia
mfumo wa tiketi za elektroniki.
Aidha,
Runyeta alisema mechi zikiwa zinapigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, basi watazamaji
watakuwa wakitumia mageti ya Uwanja wa Taifa kuingilia uwanjani hapo. Mageti
hayo ni B, C na D.
No comments:
Post a Comment