NAHODHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta ni
miongoni mwa wachezaji 30 waliotangazwa na Shirikisho la Soka la
Afrika(CAF) kuwania tuzo za mwanasoka
bora wa mwaka wa Afrika.
Samatta, ambaye ni mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa wachezaji
wa ndani kwa msimu uliopita, ameteuliwa kushindania tuzo ya mwanasoka bora wa
mwaka wa Afrika kutokana na kiwango bora anachoonesha akiwa na klabu ya KRC
Genk ya Ubelgiji.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba na TP Mazembe, amekuwa na
mchango mkubwa kwenye timu yake ya KRC Genk ambapo aliifungia timu hiyo mabao
muhimu yaliyoiwezesha kuingia kwenye mechi za mchujo za mashindano ya Europa na
kisha kuiwezesha kufuzu kuingia kwenye hatua ya makundi ya mashindano hayo.
Kwa mujibu wa mtandao wa CAF jana, Samatta anaungana na wachezaji
wengine wawili kutoka Afrika Mashariki kuwania tuzo hiyo wachezaji hao ni
Victor Wanyama kutoka Kenya anayekipiga kwenye klabu ya
Tottenham Hotspurs ya England na kipa wa kimataifa wa Uganda, Dennis Onyango wa
Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Wanyama amekuwa na msimu mzuri kwenye klabu ya Southampton na
kumpatia nafasi ya kusajiliwa kwenye klabu ya Tottenham Hotspurs msimu huu na
Dennis Onyango aliiongoza Uganda kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika lakini
pia ameiongoza Mamelodi Sundowns kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika
msimu huu.
Mbali na Samatta wengine walioteuliwa kuwania tuzo hiyo yupo
mwanasoka bora wa msimu uliopita wa Afrika, Pierre Emerick Aubameyang kutoka
Gabon ambae anaichezea Borrusia Dortmund ya Ujerumani, Riyahd Mahrez (Algeria,
Leicester City), Islam Sliman(Algeria, Leicester City).
Orodha kamili ya wanaowania tuzo hiyo ni Riyad Mahrez (Algeria, Leicester City) El Arabi Hillel Soudani
(Algeria, Dinamo Zagreb), Islam Slimani (Algeria , Leicester City) Samuel Eto’o (Cameroon, Antalyaspor),
Benjamin Mounkandjo (Cameroon na
Lorient).
Serge Aurier (Ivory Coast, PSG),
Eric Bailly (Ivory Coast, Manchester City), Yao Kouasi Gervais ‘Gervinho’ (Ivory Coast, Hebei Fortune),
Mohamed Salah (Misri, Roma), Mohamed El Neny (Misri, Arsenal),
Pierre Emerick Aubameyang
(Gabon, Dortmund).
Andre Ayew (Ghana, West
Ham), Victor Wanyama (Kenya, Tottenham),
William Jebor (Liberia, Wydad Athletic
Club), Mehdi Benatia (Morocco &
Juventus), Hakim Ziyech (Morocco, Ajax),
John Mikel Obi (Nigeria, Chelsea), Kelechi Iheanacho (Nigeria, Manchester City), Ahmed Musa (Nigeria , Leicester City).
Cedric Bakambu (DR Congo,
Villareal), Yannick Bolasie (DR Congo, Everton), Sadio Mane
(Senegal, Liverpool) , Kalidou Koulibaly
(Senegal, Napoli), Keegan Dolly (Afrika Kusini & Mamelodi
Sundowns), Itumeleng Khune (Afrika Kusini,
Kaizer Chiefs).
Mbwana Samatta (Tanzania, Genk),
Aymen Abdennour Tunisia,
Valencia), Wahbi Khazri
(Tunisia, Sunderland), Dennis Onyango
(Uganda, Mamelodi Sundowns), Khama
Billiat (Zimbabwe, Mamelodi Sundowns).
No comments:
Post a Comment