Pages

Thursday, October 20, 2016

MAKUNDI AFCON HADHARANI, UGANDA IPO KUNDI D

WAWAKILISHI wa ukanda wa Afrika Mashariki kwenye michuano ya AFCON timu ya Taifa ya Uganda imepangwa kwenye kundi la kifo katika michuano hiyo itakayofanyika nchini Gabon mwakani.

Uganda imepangwa kundi D pamoja na mataifa ya Misri, Ghana pamoja Mali hali inayoonesha kuwa wawakilishi hao wa ukanda huu wana kazi kubwa ya kufanya kama watahitaji kuvuka kwenye hatua inayofuata ya michuano hiyo.

Wenyeji Gabon wapo kundi A ambalo pia sio jepesi kwakua wamepangwa pamoja na Guinea Bissau, Burkina Faso pamoja na Cameroon.

Mabingwa watetezi timu ya Ivory coast imepangwa pamoja na Morocco, Congo DRC pamoja na Togo.

Algeria imepangwa kundi B sambamba na Tunisia, Senegal pamoja na Zimbabwe.


No comments:

Post a Comment