TIMU ya
Jeshi Stars jana imepokea kipigo cha tano mfufulizo baada ya kufungwa na KPA ya
Kenya vikapu 73 kwa 41 kwenye mashindano ya kanda ya tano uliochezwa Uwanja wa
Ndani wa Taifa.
Awali mchezo
huo ulichelewa kuanza kwa sababu Jeshi Stars walikuwa wakidaiwa ada ya ushiriki
hivyo kuzuiwa kucheza hadi walipe pesa iliyokuwa imesalia.
Baada ya
muda walilipa kiasi cha dola 180 kwani walitakiwa kulipa dola 20 kwa kila
mchezaji.
Akizungumza
na gazeti hili kocha wa Jeshi Stars, Peter Samson alisema timu yake imekuwa
ikifanya vibaya kutokana na maandalizi hafifu waliyokuwa nayo kwani walianza
mazoezi wiki mbili kabla ya kuanza kwa mazoezi.
“Sisi
tulipata barua ya kushiriki mwishoni mwa Septemba hivyo muda wa mazoezi ulikuwa
wiki mbili muda ambao ni mchache kuandaa timu”, alisema Samson.
Jeshi Stars
juzi ilifungwa na UCU vikapu 73 kwa 35, ikafungwa na USIU , UBUMWE, KCCA na leo
itacheza na Donbosco ya Tanzania kwenye mchezo wa kukamilisha ratiba.
No comments:
Post a Comment