Pages

Saturday, September 24, 2016

WABUNGE MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA UWANJANI KESHO TAIFA KUCHANGIA TETEMEKO LA KAGERA







WAKATI tiketi za elektroniki zitaanza kujaribiwa kesho, kampuni mbalimbali zimechangia jumla ya Sh milioni 20 kwa ajili ya kudhamini mchezo wa wabunge mashabiki wa Yanga na wale wa Simba utakaofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi.

Kampuni hizo ni Mwananchi Communication iliyotoa Sh milioni 10, Mfuko wa Bima ya Afya, NHIF na Jubilee Insurance, ambazo zote zimetoa Sh milioni 5 kila moja.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge, William Ngeleja ambaye pia ni mnazi wa Simba alisema matokeo ya mchezo wa kesho ni ishara ya matokeo ya mchezo wa Oktoba Mosi.

Kwa upande wa tiketi za elektroniki zitaanza kutumika leo katika mechi ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga kama majaribio kabla ya kuanza kutumika rasmi Oktoba Mosi katika mchezo wa wapinzani  Simba na Yanga.

Akizungumza jana, Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom ambayo ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamia mfumo huo, Gallus Runyeta alisema kadi  hizo zitatolewa bure katika mchezo wa leo ikiwa ni  majaribio na kuangalia dosari ambazo zitajitokeza kabla ya kuanza kuzitumia rasmi.

Akizungumzia jinsi ya kuitumia kadi hiyo, Runyeta alisema “Utajisajili kwa kupiga *150*50# halafu ni lazima uiwekee pesa kwa Airtel au M-Pesa.

Kiwango cha chini cha kuongeza salio ni Sh 1,000….: “ “Unaweza ukanunua mechi moja kwa kuandika tarehe na mchezo husika au ukachagua baadhi ya mechi au ukanunua mechi zote za msimu za timu unayoipenda.

Aliongeza: “Mbali na kadi hizo kuzitumia uwanjani, pia aliyenayo anaweza kuitumia kwa matumizi mengine kama vile kuhifadhi na kutoa fedha kwa wakala, lakini pia inamwezesha mtu huyo kulipia bidhaa na huduma mbalimbali bila kuwa na fedha mfukoni,” alisema.
Kwa upande  wa Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan 'Zungu' alisema

No comments:

Post a Comment