Pages

Monday, September 5, 2016

MEYA WA ILALA AIPIGA TAFU ASHANTI UNITED








MEYA wa Manispaa wa Ilala, Charles Kayeko ameipongeza Ashanti United kwa mafanikio waliyonayo na kuwapa msaada wa milioni tano toka mfuko wa meya.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya mandalizi ya timu hiyo toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Ashanti United, Almas Kasongo, meya Kayeko alisema Manispaa ipo pamoja na wao na itakuwa inatenga bajeti ya michezo kila mwaka.
"Michezo ndio iliyosaidia nchi hii kutafuta uhuru na mimi Meya natamani tuwe na timu ya soka kama ile ya Kampala au Nairobi ambazo zinatangaza majiji yao kimataifa na nyie mnafahamu Ilala ndio Tanzania", alisema Kayeko.
Pia Kayeko alionesha wazi dhamira aliyonayo ya manispaa hiyo kumiliki timu kama ilivyo Mbeya City kusema ameshaanza mchakato wa kutafuta timu na kuahidi kulifikisha kwenye baraza la madiwani swala la Ashanti na endapo watakubalia basi chaguo lao litakuwa Ashanti kwani ni timu ya Ilala na chimbuko lake ni Ilala.
Awali akisoma taarifa Makamu Mwenyekiti wa Ashanti United, Almas Kasongo alisema timu yao inakabiliwa na mandalizi ya ligi daraja la kwanza inayotarajiwa kuanza Septemba 24 na kusema ili iweze kucheza ligi inatakiwa kuwa na milioni 100.
"Mpaka sasa tuna milioni 24 na ili tucheze ligi tunatakiwa kuwa na mil 100 hivyo pungufu ni milioni 76", alisema Kasongo
Pia Kasongo alisema bodi na kamati ya utendaji ya timu hiyo imejitahidi kuomba msaada kwa watu mbalimbali na kilichopatikana ni hizo milioni 24 hivyo wanahitaji msaada zaidi.
Ashanti United ilishawahi kushiriki ligi kuu 2004-2007 na kushuka ligi daraja la kwanza 2008 hadi 2012 na ikapande tena ligi Kuu 2013-14 na kushuka hadi leo

No comments:

Post a Comment