MANCHESTER UNITED YAFUNGWA 2-1 NA MAN CITY
KOCHA wa Manchester
City, Pep Guardiola leo amepata ushindi wa kwanza kwenye Ligi Kuu dhidi ya
kocha mzoefu wa ligi hiyo, Jose Mourinho wakati timu yake ilipocheza na
Manchester United.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa
Old Trafford, Manchester City ilistahili kuondoka na ushindi wa mabao 2-1
kutokana na kuonesha kiwango kikubwa.
Kevin de Bruyne alifunga bao la kuongoza kwa
City katika dakika ya 15 kabla Kelechi Iheanacho hajafunga la pili katika
dakika ya 36.
Baada ya bao hilo, City ilimiliki mpira karibu
kwenye idara zote dhidi ya kikosi cha Mourinho Manchester United kwa karibu
dakika zote 45 za kipindi cha kwanza.
United ilionekana kuzinduka dakika tatu kabla ya
mapumziko kwa bao la Zlatan Ibrahimovic lililotokana na makosa ya kipa wa City.
Ushindi huo unamfanya Guardiola kuwa kocha wa
nne kushinda mechi nne za mwanzoni mwa msimu katika Ligi Kuu, kabla yake
alifanya hivyo Mourinho, Guus Hiddink na Carlo Ancelotti.
Upinzani wa muda mrefu kati ya kocha wa zamani
wa Real Madrid, Mourinho na kocha wa zamani wa Barcelona, Guardiola ulimaanisha
kwamba mechi hii ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka tangu ratiba
ya ligi ilipotangazwa.
Baada ya mechi hiyo kocha wa Manchester City,
Guardiola alisema: "Tunafuraha, nadhani watazamaji wamefurahia, kipindi
cha kwanza tulikuwa wazuri lakini kipindi cha pili mechi ilikuwa ngumu,
tulishambulia lakini hatukumalizia nafasi,”.
Naye kocha wa Manchester United, Mourinho
alisema: "Vipindi viwili vilikuwa tofauti kabisa, katika kipindi cha
kwanza hatukuwa kwenye kiwango cha kucheza mechi, kipindi cha pili kilikuwa
tofauti kabisa, tulikuwa timu ambayo tulistahili kubadili matokeo, tulistahili
kupata bao kipindi cha kwanza,”.
mwisho.
No comments:
Post a Comment