Pages

Saturday, September 17, 2016

KICHUYA AIPA SIMBA RAHA TAIFA NA YANGA YAIFUNGA MWADUI 2-0






MSHAMBULIAJI wa Sinba, Shiza Kichuya amepeleka furaha Msimbazi baada ya kufunga bao ambalo limeifanya Simba kuondoka na pointi tatu wakati ikipambana dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru.
Kichuya alipachika bao dakika ya 70 na kufanya awe na mabao mawili kwenye ligi msimu huu huku la kwanza akiwa alilifunga kwenye mchezo wa ufunguzi wa dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa.
Simba inafikisha pointi 13 na kuongoza msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi 5 ikiwa imeshinda mechi zake 4 na kutoka sare kwenye mchezo mmoja. Kabla ya mchezo wa leo, timu zote (Azam na Simba) zilikuwa zinalingana kwa kila kitu kuanzia pointi, magoli ya kufunga na kufungwa.
Azam FC waliokuwa wenyeji wa mchezo huo wamepoteza mechi kwa mara ya kwanza baada ya kucheza mechi  tano na kufikisha pointi 10 kwenye msimamo wa ligi.



Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa September 17, 2016
CCM Kambarage, Shinyanga: Mwadui 0-2 Yanga
Sokoine Stadium, Mbeya: Mbeya City 0-0 Prisons 
Manungu Complex, Morogoro: Mtibwa 2-0 Kagera Sugar
Ruvu Shooting 1-2 Mbao FC
Majimaji 1-2 Ndanda FC


No comments:

Post a Comment