Pages

Saturday, September 24, 2016

ASHANTI UNITED YAANZA VEMA MBIO ZA KUWANIA KUREJEA LIGI KUU KWA KUIFUNGA PAMBA 1-0






TIMU ya Ashanti United jana imeanza vema mbio za kuwania kupanda ligi kuu baada ya kuifunga Pamba FC, bao 1-0, kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kwenye mchezo huo kila timu ilianza kucheza kwa tahadhari huku kila mmoja akijaribu kushambulia lakini Ashanti United ndio ilifanikiwa kupata bao dakika ya 41 lililofungwa na Abeid Kisiga akiwa nje ya eneo la 18 kwa shuti kali.
Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko ambayo yaliisaidia Pamba kuliandama ango la Ashanti kwa kipindi chote lakini mabeki na kipa wa Ashanti walifanya kazi nzuri kwa kuondoa hatari zote.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kumalizika kwa mchezo, kocha wa Ashanti United, Maalim Swalehe alishukuru kwa ushindi mwembamba waliopata na kuwatupia lawama wachezaji wake kuwa wamecheza chini ya kiwango.
“Nashukuru tumepata pointi tatu lakini wachezaji wameniangusha kwa sababu wamecheza tofauti na maelekezo yangu hali iliyosababisha mchezo kuwa mgumu kwani tulikuwa na uwezo wa kushinda zaidi ya mabao tatu.
Kesho Coastal Union itaialika Polisi Moro kwenye Uwanja wa Mkwakwani  na Kimondo dhidi ya Mbeya Warriors Uwanja wa Vwawa. Jumatano Septemba 26, 2016 Mshikamano itacheza na Friends Rangers kwenye Uwanja wa Karume wakati Jumanne kwenye uwanja huohuo Polisi Dar itacheza na Kiluvya Utd.

No comments:

Post a Comment