SWANSEA CITY WAVUNJA BENKI NA KUWEKA REKODI YA KUMSAINI BORJA BASTON WA ATLETICO MADRID
Swansea City wamevunja Rekodi ya Klabu yao kwa kumsaini Straika kutoka Spain Borja Baston kutoka Atletico Madrid kwa Pauni Milioni 15.
Borja, mwenye Miaka 23, alifunga Bao 18 kwenye La Liga Msimu uliopita akiwa kwa Mkopo na Eibar.
Dau la kumnunua Borja limiezidi lile la Mwaka 2013 Swansea walipomnunua Wilfried Bony.
Borja
amekuja wakati muafaka baada ya Swansea kuondokewa na Mafowadi Andre
Ayew alieenda West Ham, Alberto Paloschi, Eder na Bafetimbi Gomis.
Hivi
Juzi Swansea pia walimchukua Mchezaji mwingine wa Spain Fernando
Llorente na hadi sasa Kocha Mpya Francesco Guidolin ameshasaini
Wachezaji Watano na wengine ni Beki wa Holland Mike van der Hoorn, Winga
wa Holland Leroy Fer na Kipa wa Australian Mark Birighitti.
No comments:
Post a Comment