DILI YA PAUL POGBA KWENDA MAN UNITED YAIVA
RIPOTI
zimevuja kuwa Manchester United wamefikia hatua nzuri katika Dili yao
na Mabingwa wa Italy Juventus na sasa watakamilisha Uhamisho wa Dau la
Rekodi ya Dunia kwa kumnunua Kiungo Paul Pogba ndani ya Masaa 48.
Ripoti
hizo zimedai Man United wametoa Ofa mpya ya Euro Milioni 110 na Euro
Milioni 10 juu ikiwa ni nyongeza mbalimbali [Jumla Pauni Milioni 100]
huku Juve waking’ang’ania kupewa Euro Milioni 5 ya ziada endapo Pogba
ataongeza Mkataba na Man United. Pia kile kikwazo cha Wakala wa Pogba, Mino Raiola, cha kutaka kulipwa Mgao wa Euro Milioni 20 kutoka kwenye Ada ya Uhamisho ambazo Juve walitaka Man United walipe zote na si kukatwa kwenye Dau lenyewe sasa inaelekea kimekwisha kwa maelewano kati ya Raiola na Man United.
Kukamilika
kwa Dili hii kutaleta afueni kubwa kwa Juve kwani Juzi waligongwa Euro
Milioni 90 walipomnunua Straika wa Argentina, Gonzalo HiguaÃn, kutoka
Napoli. Pogba aliondoka Man United Mwaka 2012 bila Ada ya Uhamisho baada ya kugomea Mkataba mpya na Man United ikaambua Pauni 800,000 tu kama Fidia ya kukuza kipaji chake.
Akiwa na Juve, Pogba alipanda chati na kuwa nguzo kubwa ya Juve akiwabeba kutwaa Ubingwa wa Serie A kila Mwaka katika Miaka yake yote Minne.
Dau la Uhamisho la Pogba litavunja zile Rekodi za Dunia za kuhamia Real Madrid za Gareth Bale, toka Tottenham kwa Pauni Milioni 85, na Cristiano Ronaldo toka Man United kwa Pauni Milioni 80.
Wengine ni Zlatan Ibrahimovic, Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan.
Pogba’s agent Mino Raiola is negotiating with Manchester United
Post a Comment