Arone Nyanda, Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Yanga |
KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), a (TFF), iliyopewa mamlaka ya kusimamia
uchaguzi wa Klabu ya Yanga imeridhishwa na mwenendo wa wanachama kwa namna
wanavyochukua na kurejesha fomu.
Katika kikao chake cha kufanya tathmini kilichoketi jioni ya leo chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Msomi Alloyce Komba kutokana na mipango yake, imesogeza mbele mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu mpaka Jumatatu Juni 6, saa 10:00 jioni. Isipokuwa Jumamosi na Jumapili ya Juni 4 na 5.
Hadi sasa wanachama tisa wamechukua na kurejesha fomu. Wanachama hao ni Aaron Nyanda na Titus Osoro wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 inayotambulika serikalini hadi sasa.
Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’, Omari Said kutoka Zanzibar ambao wanawania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Juni 25 na fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji.

No comments:
Post a Comment