Siku
kadhaa baada ya Manchester United kumfukuza aliyekuwa kocha wa klabu
hiyo, Louis Van Gaal na kumchukua kocha wa zamani wa Chelsea, Jose
Mourinho, nahodha wa Man United, Wayne ametoa maoni yake kumhusu kocha
huyo
Rooney
alimtaja Mourinho kama moja ya makocha bora na anaamini katika uwezo
wake hivyo anaamini ataweza kuisaidia klabu hiyo kurudi katika ubora
ambao ilikuwa nao awali.
“Ni
moja kati ya makocha bora duniani na anaijua vizuri Ligi Kuu ya
Uingereza. Kwangu na hata wachezaji wengine wa Manchester United huu ni
muda mwafaka. Nalisubiri kwa hamu,” alisema Rooney.
No comments:
Post a Comment