MANCHESTER UNITED KUTAFUTA 4 BORA, LEICESTER KUPEWA KOMBE LA UBINGWA
WAKATI
MABINGWA WAPYA LEICESTER CITY wakikabidhiwa Kombe Jumamosi Uwanjani
kwao King Power Stadium kwenye Mechi yao na Everton, Manchester United,
Vigogo waliotwaa Ubingwa wa BPL, Ligi Kuu England, mara nyingi zaidi,
mara 13, wapo Ugenini kusaka nafasi finyu ya kufuzu 4 Bora. Leicester,chini
ya Meneja Mtaliana ambae sasa anaitwa Muungwana, ‘El Signore’ Claudio
Ranieri, wametwaa Ubingwa wa BPL Majuzi huku wakiwa na Mechi 2 mkononi
baada ya Wapinzani wao wa karibu Tottenham Hotspur Majuzi kutoka Sare
2-2 na waliokuwa Mabingwa Chelsea.
Tayari Leicester na Spurs
zipo 4 Bora na kuacha Nafasi za 3 na 4 kugombewa na Timu kudhaa ili
kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, Msimu ujao.
Moja
ya Timu hizo ni Man United ambao ndio watafungua dimba la Mechi za
Wikiendi Ugenini huko Carrow Road kucheza na Norwich City, Timu ambayo
walifungwa nayo Mwezi Desemba Old Trafford 2-1, na ambayo sasa
inapigania.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumamosi Mei 7
14:45 Norwich v Man United
[Saa 11 Jioni]
Aston Villa v Newcastle
Bournemouth v West Brom
Crystal Palace v Stoke
Sunderland v Chelsea
West Ham v Swansea
19:30 Leicester v Everton
No comments:
Post a Comment