NDOTO ya Mshambuliaji wa Kimataifa
wa Tanzania Mbwana Samatta kucheza michuano ya Europa Ligi msimu ujao imetimia
baada ya jioni ya klabu yake ya KRC Genk kufuzu hatua ya mtoano kufuatia
kuifunga Charleroi kwa mabao 5-1 katika mchezo mkali wa marudiano uliochezwa
katika uwanja wa Cristal Arena.
Mabao yaliyoipa ushindi huo mnono
KRC Genk yamefungwa na Nikos Karelis aliyefunga mabao matatu (20,56,71),Mbwana
Samatta (27) na Sandy Walsh (45).Bao la kufutia machozi la Charleroi limefungwa
dakika ya 40 na Jeremy Perbet.
Dakika ya 16 na Charleroi ilipata
pigo baada wachezaji wake wawili Nikolas Pennetaeu na Baby kulimwa kadi
nyekundu na kulazimika kumaliza mchezo ikiwa na wachezaji tisa.
Kwa matokeo hayo KRC Genk imeshindwa kwa jumla
ya mabao 5-3.Katika mchezo wa kwanza Charleroi ilishinda kwa mabao 2-0.
No comments:
Post a Comment