FC
BARCELONA wameibuka kidedea kwenye Fainali ya 114 ya Kombe la Mfalme wa
Spain, maarufu kama Copa del Rey, kwa kuwabwaga Sevilla 2-0 kwenye
Mechi iliyochezwa Jana Jijini Madrid kwenye Uwanja wa Nyumbani wa
Atletico Madrid uitwao Estadio Vicente Calderon na kudumu Dakika 120
kufuatia Sare ya 0-0 katika Dakika 90 za kawaida. Kwenye
Mechi hii, Barca walicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 36 kufuatia Javier
Mascherano kupewa Kadi Nyekundu kwa kumvuta Jezi Kevin Gameiro aliekuwa
akichanja mbuga kwenda kufunga. Nao
Sevilla walimpoteza Ever Banega kwa Kadi Nyekundu mwishoni mwa Dakika
90 na pia Daniel Carrico alietolewa mwishoni mwa Dakika za Nyongeza 30. Ndani
ya Dakika 90 zilizoisha 0-0, Sevilla, ambao Jumatano iliyopita huko
Basel, Uswisi waliibwaga Liverpool 3-1 na kutwaa UEFA EUROPA LIGI kwa
mara ya 3 mfululizo, wangeweza kufunga katika Dakika ya 50 kama si
uhodari wa Beki wa Barca Gerard Pique alieokoa Shuti la mbali la Ever
Banega ambalo likagonga Posti. Hadi Dakika 90 Bao zilikuwa 0-0 na kila Timu kubaki Mtu 10. Katika Dakika za Nyongeza 30, Barca walipachika Bao zao za ushindi kwenye Dakika za 97 na 122 kupitia Jordi Alba na Neymar.
Hii
ilikuwa ni Fainali ya 37 ya Copa del Rey kwa Barca, wakipitwa tu na
Real Madrid waliocheza 39, na kati ya hizo 37 Barca wameshinda 28.Na
hii ni mara yap Ili mfululizo kwa Barca kuzoa Ubingwa wa La Liga pamoja
na Copa del Rey kwani Mwaka Jana, Barca walitwaa Kombe hili kwa
kuifunga Athletic Bilbao 3-1.
Timu hizi zitakutana tena mwanzoni
mwa Msimu ujao kugombea Supercopa de España kwa vile Barcelona ndio
Mabingwa wa La Liga kwa Msimu wa 2015/16. Kawaida Kombe hilo hugombewa na Bingwa wa La Liga na aliebeba Copa del Rey.
AFCON SASA KUFANYIKA BAADA YA MIAKA MINNE
-
FAINALI za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) zitakuwa zikifanyika kila
baada ya miaka minne, huku Shirikisho la Soka Afrika (CAF) likitambulisha
michuano...
Stronger Together. Ready for 2026.
-
*@Pictures by Mobila Safaris Team-Serengeti.*
*Stronger Together. Ready for 2026.*
Dear Partner,
As 2025 draws to a close, we want to thank you for...
Post a Comment