Azam FC imepokwa pointi tatu na mabao matatu kutokana na kumtumia beki wao, Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za njano.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Alfred Lucas, amesema katika mechi namba 156 iliyozikutanisha Mbeya City
dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Azam ilimchezesha Nyoni
kinyume na sheria huku wakitambua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
“Azam wamepoteza mchezo huo na sasa Mbeya City imepewa pointi tatu na
mabao matatu, pia tumewapa onyo benchi la ufundi la Azam kuwa makini
ili jambo hili lisitokee tena,” amesema afisa habari wa TFF Alfred
Lucas.
Kwa matokeo hayo sasa Simbsa inashika nafasi ya pili huku Yanga wakiendelea kuongoza ligi.
No comments:
Post a Comment