ARSENE WENGER AINGIA SOKONI KUMSAINI GRANIT XHAKA KUTUA EMIRATES
Arsenal wanakaribia kumsaini Kiungo na Kepteni wa Timu ya Germany Borussia Monchengladbach Granit Xhaka.
Tayari Klabu hizo mbili zishafikia
maafikiano kuhusu Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Switzerland kwa Dau
linaloaminika kuwa ni Pauni Milioni 30.
Xhaka, mwenye Miaka 23,
tayari yupo Jijini London kukamilisha makubaliano ya maslahi yake
binafsi pamoja na upimwaji afya yake ambao umepangwa kufanyika Wikiendi
hii.
Kutua kwa Granit Xhaka kutaimarisha safu ya Kiungo ya Arsenal
ambayo sasa itaondokewa na of Mikel Arteta, Tomas Rosicky na, pengine,
Mathieu Flamini.
Nyota
huyo anakuwa Mchezaji wa kwanza kununuliwa na Arsene Wenger ambae Msimu
uliopita alishangaza wengi kwa kutonunua Mchezaji yeyote wa mbele mbali
ya Kipa Petr Cech.
Xhaka alitua Borussia Monchengladbach Miaka Minne iliyopita baada ya kung’ara mno akiwa na Klabu ya Nchini kwake FC Basel.
No comments:
Post a Comment