Wayne
Rooney anaweza kuwemo Kikosini kwenye Mechi ya Marudiano ya FA CUP
dhidi ya West Ham hapo Jumatano huko Upton Park baada ya Jana Usiku
kurejea dimbani kuichezea Timu ya Vijana ya U-21 yao.
Huku Meneja wa Man United Louis van Gaal akiwa Jukwaani Old Trafford, Rooney alicheza Mechi hiyo kwa Dakika 61.
Rooney amekuwa nje ya Uwanja tangu Februari 13 alipoumia walipofungwa na Sunderland na kuzikosa Mechi 12 za Man United.
Van Gaal ameshadokeza kuwa Rooney, mwenye Miaka 30, atacheza Mechi hii ya FA CUP dhidi ya West Ham ikiwa yuko fiti.
Kwenye Mechi hiyo ya U-21 dhidi ya Middlesbrough, Rooney hakuwika sana ila alikaribia kufunga kwa frikiki iliyopaa kidogo juu ya mwamba wa Goli.
Man United waliifunga Boro 1-0 kwa Bao la Paddy McNair.
Baada ya kuchapwa 3-0 huko White Hart Lane Jumapili na Tottenham kwenye Mechi ya BPL, Ligi Kuu England na kuwaacha wakiwa Nafasi ya 5 kwenye Ligi hiyo, Van Gaal ameionya Difensi yake kuwa makini watakapoivaa West Ham na hasa Sentafowadi wao Andy Carrroll ambae Jumamosi alipiga Hetitriki walipotoka 3-3 na Arsenal Uwanjani Upton Park.
Van Gaal ameeleza: "Nimeiona shoo ya Carroll. Nadhani tatizo letu na Tottenham lilikuwa kutoelewana kwa Difensi yetu!"
West Ham na Man United zimelazimika kurudiana kwenye Raundi ya 6 ya FA CUP baada ya kutoka 1-1 huko Old Trafford.
Mshindi wa Mechi hii atatinga Wembley kucheza na Everton kwenye Nusu Fainali.
RATIBAJumatano Aprili 13
2100 West Ham v Man United (FA CUP)

No comments:
Post a Comment