PENATI YA DAKIKA ZA LALA SALAMA YA BENTEKE YAWAPA USHINDI LIVERPOOL
Liverpool, wakicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 62, walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuifunga Crystal Palace 2-1 huko Selhurst Park katika Mechi ya Ligi Kuu England, BPL.
Palace walitangulia kufunga Dakika ya 48 kwa Bao la Joe Ledley na ilionekana kama watashinda kilaini baada ya Liverpool kubaki Mtu 10 kufuatia James Milner kupewa Kadi Nyekundu Dakika ya 62 kufuatia Kadi za Njano 2.
Hata hivyo, Liverpool walisawazisha Dakika ya 72 baada ya Kipa wa Palace McCarthy kuteleza na kumzawadia Roberto Firmino Bao laini na kupata Bao la ushindi katika Dakika za Majeruhi kwa Penati ambayo iliashiriwa na Mshika Kibendera licha ya Beki Delaney kuonekana kutomgusa Christian Benteke ambae yeye mwenyewe ndio alifunga Penati hiyo.
Coutinho na Sturridge kuanzia kwenye benchi
VIKOSI:
Crystal Palace wanaoanza XI: McCarthy, Ward, Dann, Delaney, Souare, Jedinak, Ledley, Zaha, Cabaye, Bolasie, Adebayor
Palace akiba: Speroni, Lee, Gayle, Mutch, Sako, Chamakh, Kelly
Liverpool wanaoanza XI: Mignolet, Flanagan, Lovren, Sakho, Moreno, Milner, Henderson, Can, Lallana, Firmino, Origi
Liverpool akiba: Clyne, Toure, Benteke, Coutinho, Sturridge, Allen, Ward
Post a Comment