Wadau
wa Soka la England sasa wameanza kukubali kuwa Leicester City wana
nafasi kubwa kutwaa Ubingwa hasa baada ya kuzichapa Liverpool na
Manchester City na kupaa kileleni mwa Ligi Kuu England Pointi 5 juu ya
Timu ya Pili Tottenham Hotspurs.
Kitu kikuu ambacho kitawasaidia sana kutwaa Ubingwa ni kutokana na wao kuwa na Mechi za Ligi pekee tofauti na Wapinzani wao wengine ambao wanakabiliwa na Mashindano ya Makombe mengine kama vile FA CUP, CAPITAL ONE CUP, UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI.
Wakati wengine, wakati mwingine, wakicheza Mechi 2 au 3 kwa Wiki, Leicester wao watacheza Mechi 1 tu kwa Wiki. Mbali ya hilo, staili ya uchezaji ya Leicester ni tofauti kabisa na Wapinzani wao wakubwa, Manchester City, Arsenal na Tottenham, ambao humiliki Mpira kwa Wastani wa Asilimia 55 kwa Mechi wakati Leicester ni Asilimia 44 huku silaha yao kubwa ikiwa staili ya kaunta-ataki Tegemeza lao kubwa la mfumo wao huko, chini ya Meneja wao Claudio Ranieri, ni Wachezaji wawili hatari.
Sentafowadi wao Jamie Vardy ndie mashine yao ya Magoli Siku zote akiwa tayari kupokea Pasi ndefu toka nyuma na kuchanja mbuga kwenda Golini kufunga.
Yupo Winga wao Riyad Mahrez, kutoka Algeria, ambae hucheza Kulia na kuingia ndani na kutia Pasi kwa Mguu wake hatari wa Kushoto na pia kuifungia Magoli. Lakini pia wanae Okazaki ambae mara nyingi humsaidia Vardy katika mashambulizi akitokea kwenye Kiungo ambako pia Leicester huwatumia Danny Drinkwater na N'Golo Kante. Kwenye Difensi, kama Masentahafu, wapo Wes Morgan na Robert Huth, ambao ni nadra sana kwao kupanda juu sawa na Mafulbeki wao, na hasa Marc Albrighton, ambao hujaa kati badala ya kushika nafasi kwenye Winga.
Mechi inayofuata kwa Leicester City ni Jumamosi Ugenini na Arsenal ambayo iko Nafasi ya 3 ikiwa Pointi 5 nyuma ya Vinara hao.
Katika Mechi ya kwanza huko King Power Stadium, Arsenal iliichapa Leicester Bao 5-2.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumamosi 13 Februari 2016
15:45 Sunderland v Man United
[Mechi kuanza Saa 12 Jioni]
Arsenal v Leicester
Bournemouth v Stoke
Crystal Palace v Watford
Everton v West Brom
Norwich v West Ham
Swansea v Southampton
Chelsea v Newcastle
Jumapili 14 Februari 2016
16:30 Aston Villa v Liverpool
19:00 Man City v Tottenham

No comments:
Post a Comment