Pages
▼
Monday, January 18, 2016
YANGA YAMREJESHA NIYONZIMA KIKOSINI
Haruna Niyonzima ameuomba msamaha uongozi na wanachama wa Yanga SC kwa kosa la kuchelewa kujiunga na kambi.
Mwezi uliopita, Yanga SC ilitangaza kuvunja Mkataba na Nahodha huyo wa Rwanda kwa tuhuma za kukiuka vipengele vya Mkataba wake.
Katika Mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Niyonzima ameomba msamaha ili arejeshwe kundini.
Alisema kulitokea kutoelewana kimawasiliano na ofisi ya Katibu Mkuu, Dk Jonas Tiboroha kiasi cha kulifikisha suala hilo kwenye hatua hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amesema kwamba suala la Niyonzima limefika katika uongozi mkuu wa klabu na lipo katika hatua nzuri.
Yanga SC ilitangaza kuvunja Mkataba na Niyonzima, baada ya kuchelewa kurejea klabuni kufuatia kuruhusiwa kwenda kuichezea Rwanda katika Kombe la CECAFA Challenge nchini Ethiopia Novemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment