WAYNE ROONEY MCHEZAJI BORA ENGLAND 2015, AZOA TUZO MARA YA PILI MFULULIZO
KEPTENI
wa Manchester United, Wayne Rooney, ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa
Mwaka kwa 2015 akitetea tena Tuzo ambayo pia aliipata 2014.
Hii ni mara ya 4 kwa Rooney kuzoa Tuzo hii ambayo Wachaguaji wake ni Masapota wa Timu ya Taifa ya England.
Mapema
Desemba England ilianika Listi ya Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa
Mwaka kwa Nchi yao ambapo pia ipo Tuzo kwa Chipukizi Vijana wa chini wa
Miaka 21, U-21.
Kepteni wa England, Wayne Rooney, ambae alishinda Tuzo hiyo Mwaka Jana, ni miongoni mwa Wachezaji Watano waliokuwa wakiigombea.
Rooney
Mwaka 2015 aliiongoza England kufuzu kuingia Fainali za Mataifa ya
Ulaya, EURO 2016, ambazo zitachezwa huko France Mwezi Juni huku
akihakikisha England inashinda Mechi zao zote 10 za Kundi lao na
kuifungia Jumla ya Bao 5 kwa Mwaka 2015 kwa England huku pia akiivunja
Rekodi ya Sir Bobby Charlton ya Ufungaji Bora katika Historia ya England
kwa kufunga Bao 50 Rekodi ambayo iliwekwa na Charlton Mwaka 1968
alipofunga Bao lake la 49.
No comments:
Post a Comment