SIMBA leo imezidi kuwapa raha mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya African Sports Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huku Yanga ikilala mabao 2-0 mbele ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Ushindi wa Simba ulipokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wa
timu hiyo na umeifanya iendeleze rekodi nzuri ya ushindi katika mechi zake tatu
mfululizo sasa
Wiki za hivi karibuni Simba ilimuondoa kocha wake Dylan Kerr
na kocha wa makipa, Iddi Salim kwa kilichoelezwa
timu haichezi vizuri na jukumu kukabidhiwa Mganda Jackson Mayanja, ambaye
alikuwa Kocha Msaidizi.
Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Simba katika ligi hiyo
ikiwa chi ya Mayanja baada ya mchezo wa kwanza kuifunga Mtibwa Sugar bao 1-0
wiki mbili zilizopita, lakini ni wa tatu mfululizo kwa kocha huyo baada ya
Jumamosi wiki iliyopita kuifunga Burkina Faso mabao 3-0 iliyopo Ligi Daraja la
Kwanza katika kuwania Kombe la Shirikisho Uwanja wa jamhuri Morogoro.
Kutokana na ushindi huo wa jana, Simba sasa imefikisha pointi
36 ikiendelea kushika nafasi ya tatu nyuma ya Azam inayoshika nafasi ya pili
ikiwa na pointi 39 na Yanga inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 39, lakini
ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa. Azam ipo nyuma mchezo mmoja.
Katika mchezo wa jana, Simba ilipata bao la kwanza dakika ya
14 mfungaji akiwa Hamisi Kiiza akimalizia krosi ya Hassan Ramadhan Kessy, kabla
ya Kessy kuifungia Simba bao la pili dakika ya 30 baada ya kuwalamba chenga
mabeki wa African Sports.
Simba iliendelea kufanya mashambulizi ya nguvu, huku Sports
wakionekana kuzidiwa kila idara, ambapo dakika ya 42 Kiiza alifunga bao la tatu
kutokana na uzembe wa beki Halfan Twenye aliyerudisha mpira kwa kipa wake na Kiiza kuunasa.
Bao hilo la Kiiza lilikuwa la 12 kwake kufunga katika msimu
huu akiendelea kuwa nyuma ya Amis Tambwe wa Yanga anayeongoza akiwa na mabao
13.
Sports ilijaribu mara chache kufurukuta, lakini umaliziaji
haukuwa mzuri, ambapo wachezaji Pera Ramadhan na Rajabu Isihaka walishindwa
kuzitumia.
Simba iliongeza bao la nne dakika ya 75 mfungaji akiwa Haji
Ugando baada ya kupokea pasi ya Kessy na kuibua shangwe kwa mashabiki wa timu
hiyo.
Wakati huohuo, Yanga jana ilipoteza mchezo wa kwanza katika
ligi ya msimu huu baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga.
Yanga na Azam zilikuwa ndiyo timu pekee katika ligi hiyo msimu
huu, ambazo hazifungwa mechi, hivyo kwa matokeo hayo imebaki Azam pekee.
Coastal ilipata bao la kwanza dakika ya 27 mfungaji akiwa Miraji Adamu kwa mpira
wa adhabu baada ya beki Kelvin Yondani kuunawa mpira na kupiga adhabu hiyo
iliyomshinda kipa Deogratias Munishi ‘Dida’.
Washambuliaji
wa Yanga wakiongozwa na Donald Ngoma walijaribu kufukuta kutaka kusawazisha bao
hilo, lakini umaliziaji ulikuwa butu.
Dakika
ya 62, Juma Mahadhi alifunga bao la pili kwa shuti kali, bao ambalo liliwaamsha
mashabiki wa Coastal, ambao matokeo hayo yamewafanya wafikishe pointi 13.
Naye
Alexander Sanga anaripoti kutoka Shinyanga kuwa Mwadui imeibuka na ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Toto Aficans mchezo uliofanyika Uwanja wa Mwadui.Bao hilo
lilifungwa dakika ya 63 na Kelvin Kongwe kwa shuti la mbali.
Hicho
ni kipigo cha nne mfululizo kwa Toto Africans baada ya kufungwa na African
Sports, Prisons na Stand United.
Mchezo
mwingine uliofanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ambapo JKT Ruvu na
Majimaji zilitoka 0-0.
No comments:
Post a Comment