MABONDIA
Sadiq Momba na Baina Mazola wamesaini mkataba wa kupigana Machi 5, katika Ukumbi wa Tasuba Bagamoyo Mkoa wa
Pwani
Akizungumza
na gazeti hili, promota wa pambano hilo Muhsin Sharif alisema pambano hilo ni
la uzani wa kg 59, na litakuwa la raundi nane.
“Nimeamua
kuwapambanisha mabondia hawa kwani ndio wanatamba kwenye uzito huo kwa ajili ya
kuleta chachu ya mchezo wa ngumi nchini”, alisema Sharif
Pia Sharif alisema Momba ni bondia maarufu ambaye anakwenda sana nje ya nchi kwa ajili ya mapambano mbali mbali na amekuwa akifanya vizuri awape nje hata hivyo mpambano wake wa mwisho nchini Thailand alipigwa kwa KO ya raundi ya tatu hivyo anahitaji ushindi na pointi za kutosha kumrudisha kileleni. Kwa upande wa Mazola katika uzito wake yeye ni namba tatu katika ngumi hapa nchini hivyo anataka kuwa zaidi ya bondia Momba Wadadisi wa ngumi wanasema Momba baada ya kupoteza mpambano wake nje ya nchi wadogo zake wamepania kucheza nae kwani inaonekana kiwango chake kimepungua. |
Pages
▼
No comments:
Post a Comment