Shirikisho la soka la mpira wa miguu ulimwenguni FIFA limeachia adhabu waliyopewa klabu za Real Madrid na Atletico kuwa huru kwa usajili hadi hapo zitakapo sikilizwa rufani zao na shirikisho hilo.
Klabu zote mbili ziliandika katika taarifa zao kuwa FIFA wameziachia huru kuendelea na usajili wa wachezaji mara baada ya kufungiwa kufanya hivyo kutokana na kufanya usajili wa watoto, kinyume na utaratibu.
Real Madrid na Atletico wote waliwasilisha rufani zao kwa shirikisho hilo na sasa wataendelea kua huru hadi hapo FIFA itakapopitia upya kesi yao na kufanya maamuzi.
Adhabu kama hiyo iliwakumba FC Barcelona mwaka 2014 na kufeli katika rufaa yao, kitu kilichopelekea klabu hiyo isajili wachezaji Arda Turan na Alex Vidal ambao imeanza kuwatumia mwezi huu wa January mara baada ya kumaliza kifungo.
No comments:
Post a Comment