
Hivi sasa, Man United, chini ya Meneja Louis van Gaal ambae ameshaanza kukumbwa na manung’uniko ya Washabiki, wapo kwenye wimbi la Mechi 5 bila ushindi.
Mara ya mwisho Man United kushinda ni Novemba 21 walipoifunga Watford 2-1 kwa Bao la ushindi la kujifunga mwenyewe Troy Deeney katika Dakika ya mwisho ya Gemu hiyo.
DONDOO MUHIMU:
-Man United wameifunga Norwich kwa Bao 4-0 katika Mechi 3 zilizopita zilizochezwa Old Trafford.
-Mechi hizo ni Ligi Kuu England, Machi 2013, Ligi Cup Oktoba 2013 na Ligi, Aprili 2014.

Mwaka 1996 pia walitwaa Ubingwa baada ya Msimu huo kwenda Mechi 5 mfululizo bila ushindi katika Mechi za Ligi.
Mara zote hizo 3, Man United ilikuwa chini ya Meneja Lejendari Sir Alex Ferguson alietwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 13 kwenye Misimu ya 1992–93, 1993–94, 1995–96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11 na 2012–13.
Wanatakwimu wamedai wimbi la sasa pia haliwezi kuwaathiri kwa vile Timu zinapoteza Pointi kila kukicha na wao bado wapo nafasi nzuri wapo Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Leicester, 4 nyuma ya Timu ya Pili Arsenal na 3 nyuma ya Timu ya 3 Man City.
Mechi zinazofuata kwa wikiendi ni Leicester kucheza Ugenini na Everton na Arsenal kuikaribisha Man City huko Emirates.
No comments:
Post a Comment