Pages

Wednesday, November 11, 2015

SAMATTA AWASILI AWAPA NENO WACHEZAJI WA TANZANIA

Mbwana Samata akisaliamiana na baba yake mzazi Ally Samatta baada ya kutua Uwanja wa Ndege leo






MSHAMBULIAJI wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa kwenye timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mbwana Samatta amesema wachezaji wa Tanzania wanaweza kikubwa ni juhudi, malengo na kujua wanataka nini.
Akizungumza baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)  ambako Mbwana Samatta  alipokelewa na familia yao ikiongozwa na baba yake mzazi Ally Samatta pamoja na mashabiki wa soka, alisema kujituma kunaweza kukufikisha mbali zaidi hasa pale unapokuwa na nia ya dhati na mafanikio katika soka.
“Naamini baadhi ya wachezaji wa Tanzania wanaweza kuwa bora kama mimi nilivyoibuka kuwa mfungaji bora na mchezaji bora ila kinachotakiwa ni kujituma na kutambua unataka kufika wapi”, alisema Samatta
Pia Samatta alijikuta akishindwa kujizuia kuonesha furaha baada ya kukutana na familia yake ikiwa inamsubiri uwanja wa ndege  kwa ajili ya kumpongeza kwa mafanikio yake pamoja na kusalimiana nae kabla ya kuchukuliwa na uongozi wa Shirikisho la Soka kwa ajili ya kuingia kambini.
Pia Samatta alisema anatamani kama mafanikio aliyopata mama yake mzazi angeshuhudia hiki kinachoendelea.
Samatta amewaambia watanzania kuwa wamekuja kwa ajili ya mchezo dhidi ya Algeria na wanafahamu Algeria ni timu bora na ngumu barani Afrika, lakini watashirikiana na wanaweza kufanya vizuri kwenye mechi ya nyumbani huku akiamini kocha atakuwa ameiandaa timu vizuri
Samatta na Thomas Ulimwengu wamewasili nchini kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Algeria kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa  wakitokea Nairobi, Kenya ambako walikwama juzi kutokana na ndege yao kuzuiliwa kuruka kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.

No comments:

Post a Comment