Pages

Saturday, November 7, 2015

PAPA WEMBA KUTUMBUIZA LEO BAGAMOYO MUSIC FESTIVAL 2015 BAADA YA KUTUA DAR JANA


Mwanamuziki Papa Wemba (kulia) akisalimiana na mwenyeji wake waandaaji wa Tamasha la Karibu Music Festival 2015 mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie akimtambulisha kwa wenyeji wao.

Mwanamuziki Papa Wemba akiwa katika picha ya pamoja na wasanii alioambatana nao waliomo katika bandi yake mara baada ya kutua Tanzania tayari kufanya mashambulizi katika Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika Bagamoyo.


Mwanamuziki Papa Wemba akiwa katika picha ya pamoja na wasanii alioambatana nao waliomo katika bandi yake mara baada ya kutua Tanzania tayari kufanya mashambulizi katika Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika Bagamoyo.

Msafara wa mwanamuziki Papa Wemba ukipokewa na wenyeji wao mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA).

Mwanamuziki Papa Wemba (kushoto) akiwa na Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie (kulia) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA).

MWANAMUZIKI nguli wa ndansi kutoka nchini Congo (DRC) Papa Wemba amewasili usiku huu jijini Dar es Salaam tayari kwa kutumbuiza katika tamasha la Karibu Music Festival 2015. Papa Wemba ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA) majira ya saa nane kasoro na ndege ya shirika la Kenya (Kenya Airways-KQ).
Mara baada ya kuwasili msanii huyo pamoja na wanamuziki wake walipokewa na Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie pamoja na waandaaji wa Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika mjini Bagamoyo. Papa Wemba na msafara wake umeelekea Bagamoyo tayari kwa kukonga mioyo ya washabiki wa Tamasha hilo.
Wasanii wengine ambao wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo ni Jhikolaman, Isha Mashauzi, Damian Soul, Juma Nature, Barnaba, Shilole, mshindi wa pili wa BSS, Nassib Fonabo na bendi yake ya Spirit na wengine wengi. Tamasha hilo lililoanza Novemba 6 hadi 8 katika viwanja vya Mwanakalenge, Bagamoyo mkoani Pwani linalengo la kukuza muziki asili ya Afrika.

Tamasha limeandaliwa na Kampuni ya watayarishaji wa muziki ya Legendary kwa kushirikiana na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. Wadhaminiwa wengine ni pamoja na Swiss Embassy, Precion Air, Coca Cola, Mwananchi Communication, Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets. huku mgeni mwalikwa akiwa ni mwanamuziki kutoka Congo, Papa Wemba.

No comments:

Post a Comment