Pages

Saturday, November 14, 2015

HASSANOO AACHIWA KWA DHAMANA

HATIMAYE aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Pwani (Corefa), Hassan Othman maarufu kama Hasanoo (pichani juu) amepata dhamana, baada ya kusota gerezani zaidi ya miaka miwili.
Mbali na Hasanoo washtakiwa wengine ni Ally Kimwaga, Danstan Mwanga, Godfrey Mwanga, John Mlay, Khalid Fazaldin na Lusekelo Mwakajila.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya kusikiliza hoja za pande mbili kuhusiana na sakata la washtakiwa kupewa dhamana.
Hakimu Simba alisema anaunga mkono hoja za Wakili wa Hasanoo, Majura Magafu kuwa mpaka Mahakama Kuu ipokee rufaa ni lazima sababu za rufaa hiyo ziwe zimewasilishwa mahakamani.
"Upande wa Jamhuri ulizuia mchakato wa kutoa dhamana kwa washtakiwa kwa kile walichodai kuwa wanakusudio la kukata rufaa, baada ya mahakama kutoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa.
"Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kama rufaa yake itakuwa imepokelewa, basi Mahakama Kuu itaitisha jarada hili la kesi na mahakama hii ya Kisutu itakuwa haina mamlaka tena ya kusikiliza kesi hiyo, lakini mpaka sasa hamna jambo kama hilo, kwa hiyo mchakato wa dhamana unaendelea" alisema
Pia, alisema mahakama ilifamnya uchungu wa kesi mbili ambazo ziliwasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Paul Kadushi kuwa zilikuwa hazina mwisho wa uamuzi wa kutekelezwa kwa hukumu, kwa hiyo mahakama imetupilia mbali kesi hizo.
Alisema kutokana na sababu hizo mahakama inaendelea kutibisha udhamini wa washtakiwa kama ilivyotoa masharti ya dhamana kuwa kila mshtakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja wa wadhamini hao anatakiwa awe na mali isiyohamishika yenye thamani ya sh. milioni 50.
Hata hivyo, Hasanoo na baadhi ya washtakiwa wenzake walipata dhamana, baada ya kutimiza masharti hayo na kesi itaendelea kusikilizwa Novemba 17 mwaka huu.
Awali, Ilidaiwa kuwa kwa nia ovu walipanga, wakatekeleza, wakasimamia na kuwezesha kifedha kufanyika kwa biashara ya nyara za Serikali kwa kusafirisha vipande 569 vya pembe za ndovu, vyenye uzito wa kilogramu 1330 na thamani ya sh. bilioni 1.1 kwenda Hong Kong.
Kwa hisani ya Bin Zubeiry blog

No comments:

Post a Comment