Pages

Saturday, November 7, 2015

CRISTIANO RONALDO ADAI MAN UNITED ITATWAA UBINGWA ENGLAND CHINI YA MENEJA VAN GAAL

Cristiano Ronaldo amedai Klabu yake ya zamani Manchester United itatwaa Ubingwa wa England Msimu huu.
Ronaldo, ambae sasa ni Mchezaji wa Real Madrid, aliichezea Man United kwa Miaka 6 na anaamini Timu hiyo Msimu huu, chini ya Louis van Gaal, imepanda kiwango.
Akikiri kuwa yeye ni Shabiki wa Man United, Ronaldo alieleza: “Manchester ni nzuri Mwaka huu. Wako bora. Wapo juu na hii ni nzuri na ni Klabu ninayoipenda na kila Mtu anajua hilo.”
Ronaldo aliongeza: “Ninachotegemea ni Man United kuwa Mabingwa wa England. Wakiwa na Van Gaal, Wachezaji wote na Wafanyakazi wote, nawatakia kila heri.”

Ronaldo, mwenye Miaka 30, aliongea maneno hayo katika uzinduzi wa Filamu ya maisha yake ambapo pia aligusia uhusiano wake na Lionel Messi wa Barcelona ambae kila Siku hushindanishwa nae.
Hivi sasa Ronaldo ndie anaeshikilia Rekodi zote za kufunga Mabao mengi kwa Klabu, La Liga na UEFA CHAMPIONS LIGI kupita Messi.
Staa huyo ameeleza: “Watu hutulinganisha kila wakati na hii ni kawaida tangu kufananishwa. Simaanishi mimi na Messi tu lakini Watu wote hulinganishwa mkiwa shuleni. Nani mwenye kasi? Nani mwenye akili? Hiyo ni sehemu ya maisha. Hainishangazi lakini wakati mwingine hunichosha.”
Aliongeza: “Messi ni mchapakazi anaejituma. Kumshinda ni kitu safi na najua husikia raha akiona navunja rekodi yake! Nadhani tuzivunje rekodi. Pengine Miaka 10 au 20 atatokea Mtu atavunja rekodi yangu. Hakuna lisilowezekana ingawa ni ngumu!”

No comments:

Post a Comment