Rooney alianza kuichezea Timu ya Kwanza ya Everton tangu 2002, akiwa Kijana wa Miaka 17, na kwa Miaka Miwili alizoa kila sifa lakini Mwaka 2004 alihamia Man United kwa Dau la Pauni Milioni 30 na kuzua chuki toka kwa Mashabiki Goodison Park.
Rooney hana raha tena na Goodison Park ambako huzomewa na kutukanwa n ahata Magoli kwake Uwanja hapo ni nadra kwake.
Lakini Van Gaal hajakata tamaa na Jana alisema: “Pengine dhidi ya Everton wastani wake si mzuri. Sasa umefika wakati abadilishe hilo. Sijui kwa nini amekuwa na shida pengine muulizeni yeye. Mimi ni Meneja ninae tathmini wapinzani na kumpa ushauri njia bora kuvunja difensi nap engine atafunga.”
Hivi sasa Rooney sie Straika mkuu wa Kikosi cha Van Gaal baada ya jukumu hilo kupewa Chipukizi mpya Anthony Martial na Rooney kucheza nyuma yake lakini Van Gaal anaamini bado mchango wa Kepteni wake Rooney ni muhimu.
Ameongeza: “Rooney anaweza kucheza nafasi nyingi na kwangu si muhimu nani anafunga ili mradi tufunge Goli nyingi.”
Van Gaal haamini kuwa mzigo wa kuwa Nahodha umemwelemea Rooney kwani Kepteni wake huyo ana uweza kutokana na tabia yake.
No comments:
Post a Comment