CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), kinatoa pongezi za dhati kwa
Dk. John Magufuliwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Tanzania.
TASWA
imepokea kwa furaha ushindi huo wa Dk. Magufuli, ikiamini atawapa furaha
wanamichezo katika masuala mbalimbali kama alivyofanya mtangulizi wake Rais,
Jakaya Kikwete ambaye anamaliza muda wake wa kuwatumikia Watanzania kwa mujibu
wa katiba na ataanzia pale mtangulizi wake alipoishia kuhusiana na michezo kwa
ujumla.
Kutokana
na hali hiyo tunampongeza Rais Mteule Dk. Magufuli na Makamu wake, Samia Suluhu
Hassan, ambaye atakuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kushika wadhifa wa Makamu wa
Rais hapa nchini.
Tunaamini
watakuwa tumaini kubwa la wanamichezo na tunaahidi kuwapa ushirikiano wa
kutosha ili watekeleze majukumu yao ipasavyo upande wa michezo.
Pia
TASWA inawapongeza wadau wote wa michezo waliochaguliwa kwa nafasi mbalimbali
za Ubunge na Udiwani na tunaamini ushindi wao utakuwa mwanzo mzuri katika
kusaidia michezo hapa nchini.
Tunawapongeza
pia wale ambao si wanamichezo, lakini walitumia mgongo wa michezo na
wanamichezo kutafuta uongozi wa kisiasa katika nafasi za Ubunge na Udiwani,
wakiahidi watasaidia michezo. Nao tunawapongeza na tunasubiri utekelezaji wa
ahadi zao.
Wanasiasa
ndiyo wanaounda Serikali, tena wao ndio wanaofanya uamuzi kutokana na nafasi
zao. Watendaji ni wataalamu, na kazi yao ni kushauri au kutoa ushauri. Ushauri
ni kitu kimoja, na ushauri kufanyiwa kazi ni kitu kingine pia.
Hivyo
basi tunaamini wanasiasa walioingia wakitokea kwenye
michezo wanajua matatizo yaliyoko huko kwa kiasi kikubwa kuliko mwingine
yeyote, hivyo wanaweza kusaidia kwa kiasi fulani mawazo ili michezo ipige
hatua.
Ahsanteni,
Juma
Pinto
Mwenyekiti
TASWA
30/10/2015
No comments:
Post a Comment