Pages

Saturday, October 24, 2015

RATIBA, LIGI KUU ENGLAND: JUMAMOSI ARSENAL WAIPANIA VILIVYO EVERTON, JUMAPILI NI DABI YA 170 YA JIJI LA MANCHESTER KATI YA MANCHESTER UNITED vs MANCHESTER CITY.

BAADA ya kuzichapa Man United, Watford na Bayern Munich, Jumamosi Arsenal wana nafasi ya kutwaa uongozi wa Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza katika Miaka Miwili ikiwa wataifunga Evrton Uwanjani Emirates.
Msimu uliopita kwenye Mechi kama hii, Arsenal iliifunga Everton 2-0 na safari hii Arsenal wapo kwenye wimbi zuri la ushindi wakitoka kuzichapa 3-0 Man United na Watford kwenye Ligi na 2-0 Bayern Munich kwenye UEFA CHAMPIONS.
Everton wao wanatinga kwenye Mechi hii wakitoka kwenye kipigo cha 3-0 Nyumbani kwao Goodison Park kutoka kwa Man United.

Ikiwa Arsenal wataifunga Everton basi watakaa kileleni mwa Ligi pengine hadi Jumapili wakati Dabi ya Manchester ikichezwa huko Old Trafford kati ya Man United na Man City ambao wana nafasi ya kuishusha Arsenal toka kileleni.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Oktoba 24

17:00 Aston Villa v Swansea
17:00 Leicester v Crystal Palace
17:00 Norwich v West Brom
17:00 Stoke v Watford
17:00 West Ham v Chelsea
19:30 Arsenal v Everton

Jumapili Oktoba 25
15:00 Sunderland v Newcastle
17:05 Bournemouth v Tottenham
17:05 Man United v Man City 

19:15 Liverpool v SouthamptonSmalling akishangilia bao lake kwenye mchezo uliowakutanisha City na Man 

No comments:

Post a Comment