Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, October 10, 2015

JURGEN KLOPP ATAMBULISHWA LIVERPOOL


Klopp atambulishwa rasmi leo LiverpoolRasmi sasa LiverpoolMara baada ya kusaini Mktaba wa Miaka Mitatu, ukiwa na nyongeza ya Mwaka mmoja juu, na Klabu ya Liverpool, Meneja mpya wa Liverpool, Mjerumani Jurgen Klopp alitambulishwa rasmi na kuongea na Wanahabari.
Klopp amewataka Mashabiki wa Liverpool kuwa na subira ili apate muda wa kuisimika falsafa yake.
Lakini Klopp alikiri kusubiri kwa Miaka 25 kutwaa Ubingwa ni muda mrefu kwa Klabu kama Liverpool na kutoboa kuwa anategemea ndani ya Miaka Minne watatwaa Ubingwa.
Hata hivyo, Klopp amesisitiza yeye si ‘Mtu Spesho’ ila ‘Mtu wa Kawaida’ na hilo lilikuja baada ya kutakiwa kujifananisha na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ambae alijibatiza ni ‘Mtu Spesho’ katika mazungumza yake ya kwanza tu na Wanahabari alipotambulishwa kama Meneja mpya wa Chelsea Mwaka 2004.
Mechi ya kwanza kwa Klopp itakuwa hapo Oktoba 17 huko White Hart Lane dhidi ya Tottenham kwenye Ligi Kuu England.Akipata picha na Mwenyekiti wa Liverpool Tom WernerAkiwa na jezi ya Liverpoolpicha ya pamoja

No comments:

Post a Comment