Clattenburg, mwenye Miaka 40, ndie aliesimamia Dabi iliyopita Uwanjani Old Trafford wakati Man United, chini ya Meneja Louis van Gaal, ilipoinyuka City Bao 4-2 Mwezi Aprili kwa Bao za Ashley Young, Marouane Fellaini, Juan Mata na Chris Smalling
Msimu huu, Clattenburg ameshachezesha Mechi 2 za City, ambazo waliifunga Watford na nyingine kufungwa na Tottenham, na Mechi 1 ya Man United waliyoifunga Southampton 3-2.
Kwa Msimu huu, Refa huyo ameshachezesha Gemu 11 na kutoa Kadi za Njano 11 na Kadi Nyekundu 2.
WIKIENDI hii Ligi Kuu England ina Mechi kali ikiwamo Dabi ya Jiji la La Manchester wakati Manchester United wakiwa Nyumbani Old Trafford kuikaribisha Manchester Cityhapo Jumapili.
Lakini Jumamosi, Arsenal, ambao wako Nafasi ya Pili kwenye Ligi Kuu England wakiwa na Pointi 19 sawa na Man United na Pointi 2 nyuma ya Vinara Man City, wana nafasi ya kutwaa uongozi ikiwa watashinda Nyumbani kwao Emirates wakicheza na Everton.
Timu zote hizi za kileleni, City, Arsenal na Man United, zimetoka kwenye Mechi za Kati-Wiki za UEFA CHAMPIONS LIGI za Makundi yao.
Akiongelea Dabi yao, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amesema ushindi dhidi ya City ni muhimu ili kusisitiza azma yao ya kuwemo kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa Msimu huu.
Nao Arsenal wanatoka kwenye wimbi zuri la ushindi baada ya kuzichapa Man United na Watford 3-0 kila mmoja kwenye Mechi za Ligi na kisha Juzi kuifunga Bayern Munich 2-0 kwenye Mechi yao ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI.
Ikiwa Arsenal wataifunga Everton watakaa kileleni mwa Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza kwa karibu Miaka Miwili na kubakia hapo hadi Jumapili ambapo Dabi ya Manchester itaamua kama watabaki huko juu au wataporomoshwa.
Jumamosi Mabingwa Watetezi Chelsea, ambao wako Nafasi ya 11, wapo Ugenini huko Upton Park kucheza na West Ham ambayo iko Nafasi ya 3 huku Timu hizo zikitenganishwa kwa pointi 5.
Mvuto mwingine wa Wikiendi hii ni Mameneja Wawili wapya, Jurgen Klopp wa Liverpool na Sam Allardyce wa Sunderland, kucheza Mechi zao za kwanza kwenye Viwanja vyao vya Nyumbani baada ya kuanza himaya zao kwa kuwa Ugenini kwenye Ligi Wikiendi iliyopita.
Klopp alianza kwa Sare ya 0-0 huko London Uwanjani White Hart Lane walipocheza na Tottenham wakati Allardyce alichapwa 1-0 huko The Hawthorns na West Bromwich Albion.
Jumapili Liverpool wako kwao Anfield kucheza na Southampton na Sunderland wako kwao Stadium of Light kuivaa Newcastle.
No comments:
Post a Comment