ALIYEKUWA KOCHA KWENYE LIGI KUU YA UINGEREZA AJA TANZANIA KUONGOZA KITUO CHA VIJANA CHA MICHEZO
Ndugu
Ray Power, ambaye amewahi kuwa Kocha wa Chama Cha Soka na mkuu wa
kitengo cha mpira wa miguu katika chuo kiitwacho Central College
Nottingham; ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi katika Kituo cha Vijana
cha Michezo kilichopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam (pichani).
Katika nafasi yake mpya, Ndugu Power atasimamia mafunzo na Uongozi wa
kituo kipya ambacho kinategemewa kufunguliwa tarehe 19 ya Mwezi huu.
Ndugu Power anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi wa
kituo; Stewart Hall aliyejiunga na timu ya Azam kwa mara nyingine kama
Kocha Mkuu
No comments:
Post a Comment