Pages

Friday, September 18, 2015

WENGER NI MENEJA WA KWANZA ULAYA KUFUNGWA MECHI 50 UEFA CHAMPIONS LIGI

Arsene Wenger, ambae Jose Mourinho aliwahi kumbatiza kuwa ni ‘Mtu Spesho wa Kufeli’, ameweka Rekodi mpya huko Ulaya kwa kuwa Meneja wa kwanza wa Klabu aliefungwa Mechi 50 za UEFA CHAMPIONS LIGI.
Pengine Rekodi hii ya kushindwa hastahili Mtu aliefanikiwa kutwaa Ubingwa Ligi Kuu England mara 3 na kubeba FA CUP mara 6 lakini Jana, baada ya kuchapwa 2-1 huko Zagreb na Dinamo Zagreb katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi F la UEFA CHAMPIONS LIGI, Wenger ndio rasmi ameshika Rekodi ya kuwa wa kwanza kufungwa Mechi 50 katika Mashindano hayo. Huu ni Msimu wa 18 kwa Wenger kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI akiwa na Arsenal lakini hajawahi hata mara moja kubeba Kombe hilo na alifika Fainali mara moja tu.
Hata hivyo, licha ya takwimu hii ya kufungwa mara 50 kumdidimiza Wenger lakini pia inaonyesha mafanikio yake makubwa ya kuhakikisha Mwaka nenda rudi Arsenal inashiriki UEFA CHAMPIONS LIGI kitu ambacho hakikutwi na Meneja mwingine yeyote huko England kwa sasa.

No comments:

Post a Comment