Pages

Wednesday, September 16, 2015

RONALDO APIGA HAT-TRICK REAL MADRID MABAO 4-0 DHIDI YA SHAKHTAR DONETSK KWENYE UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Ndani ya Uwanja wa Uwanja wa Estadio Santiago Bernabéu, Spain Real Madrid wanaongoza kwa bao la Karim Benzema dakika ya 30 kipindi cha kwanza dhidi ya timu ya Shakhtar Donetsk katika kipindi kilichomalizika cha kwanza kwa bao 1-0. 
Real, wakiwa kwao Santiago Bernabeu, wameitandika Shakhtar Donetsk Bao 4-0 katika Mechi ya kwanza ya Kundi A la UEFA CHAMPIONS LIGI.Real walipata Bao lao la kwanza katika Dakika ya 30 Mfungaji akiwa Karim Benzema na Bao hilo kudumua hadi Haftaimu.
Katika Dakika ya 50, Taras Stepanenko wa Shakhtar Donetsk alibandikwa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

Ronaldo aliipa Real Bao la Pili kwa Penati ya Dakika ya 55 ambayo ilitolewa baada ya Shuti lake kuguswa mkononi na Darijo Srna.
Dakika ya 63 Ronaldo akafunga Bao la 3 kwa Real kwa Penati nyingine iliyotolewa baada ya Azevedo kuushika Mpira.
Ronaldo alipiga Bao lake la 3 na la 4 kwa Real katika Dakika ya 81 baada ya Shuti la Marcelo kuzuiwa na kumrudia yeye aliemalizia vizuri.
Ronaldo akishangilia moja ya bao lakeRonaldo akishangilia, alifunga bao tatu  kwenye mchezo huo

No comments:

Post a Comment