Pages

Wednesday, September 23, 2015

ROBERT LEWANDOWSKI APIGA HAT-TRICK NDANI YA DAKIKA 6 WAKATI FC BAYERN MUNICH YAIFUNGA VFL WOLFSBURG MABAO 5-1

 Robert Lewandowski Usiku huu amepiga Bao 5 ndani ya Dakika 9 na kuvunja Rekodi kadhaa za Bundesliga baada ya Timu yake kuitwanga VfL Wolfsburg Bao 5-1.
Katika Mechi hiyo iliyochezwa huko Allianz Arena huko munich, Germany, Wolfsburg waliongoza 1-0 hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili Robert Lewandowski, Mchezaji kutoka Poland mwenye Miaka 27, alitumia Dakika 4 tu kupiga Hetitriki ikiwa ndio Hetitriki iliyofungwa ndani ya muda mfupi katika Historia ya Bendesliga.
Rekodi hii ilikuwa ikishikiliwa na Mchezaji wa Duisburg, Michael Toennies, aliyoweka Mwaka 1991 kwa kufunga Hetitriki ndani ya 5.

Akishangilia moja ya bao zake leo usiku huu

Robert Lewandowski akishangilia baada ya kuipiga vilivyo Wolfsburg

Pia Lewandowski, kwa kupiga Bao 5 ndani ya Dakika 9 za Kipindi cha Pili, ameivunja Rekodi ya Jermaine Defoe wa Tottenham ya kufunga Bao 5 ndani ya Dakika 36 ya Kipindi cha Pili wakati Tottenham inaitwanga Wigan 9-1 Mwaka 2009.
Bosi wa Bayern Pep Guardiola alipigwa butwaa na Rekodi ya Lewandowski na kubaki kusema: 'Mara nyingine Soka ni Wehu!'

Lewandowski akishangilia baada ya kuifanyia maajabu timu yake na akitokea benchi
Akitupia nyavuni
Ndani ya dakika 9 Robert L. alikuwa ameshafunga bao 5 peke yake na kuipa ushindi mnono Bayern iliyokuwa nyumba ya bao 1-0 usiku huu na kuibuka kidedea kwa bao 5-1.
Daniel Caligiuri 26' 


Bayern Munich
Robert Lewandowski 51'
Robert Lewandowski 52'
Robert Lewandowski 55'
Robert Lewandowski 57

Robert Lewandowski 60

No comments:

Post a Comment