Pages

Saturday, September 19, 2015

RATIBA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI HII, NI CHELSEA vs ARSENAL, JUMAPILI NI SOUTHAMPTON vs MANCHESTER UNITED

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Septemba 19

14:45 Chelsea vs Arsenal
17:00 Aston Villa vs West Brom
17:00 Bournemouth vs Sunderland
17:00 Newcastle vs Watford
17:00 Stoke vs Leicester
17:00 Swansea vs Everton
19:30 Man City vs West Ham 

Jumapili Septemba 20
15:30 Tottenham vs Crystal Palace
18:00 Southampton vs Man United
18:00 Liverpool vs Norwich
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesem kuwa kukosa matayarisho kwa ajili ya Mechi yao ya Leo ya huko Stamford Bridge si kisingizio.
Arsenal Leo wapo huko Stamford Bridge kucheza na Mabingwa Chelsea katika Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi Kuu England Wikiendi hii ambayo itaanza Saa 8 Dakika 45 Mchana kwa Saa za Tanzania.
Timu zote hizi mbili Jumatano Usiku zilicheza Mechi za Makundi yao ya UEFA CHAMPIONS LIGI ambazo Arsenal ilifungwa 2-1 huko Croatia na Dinamo Zagreb wakati Chelsea inaichapa 4-0 Maccabi Tel Aviv Uwanjani Stamford Bridge.
Wenger ameeleza: “Situmii hilo kama kiingizio. Naamini tuko kwenye nafasi ya kufanya vizuri.”
Kwenye Mechi yao huko Zagreb na Dinamo Zagreb, alifanya mabadiliko 6 kwenye Kikosi chake kwa kuwapiga Benchi Kipa Petr Cech, Fulbeki Nacho Monreal, Kiungo Francis Coquelin na Fowadi Theo Walcott wakati Kiungo Aaron Ramsey na Fulbeki Hector Bellerin hawakuwamo kabisa Kikosini.
Wote hao sasa wanaweza kuivaa Chelsea lakini Wenger amesema hajaamua nani ataanza kama Fowadi kati ya Olivier Giroud, ambae huko Zagreb alitolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 40, au Theo Walcott.
Wenger amesema anawajibika kwa Kikosi kilichofungwa na Dinamo Zagreb lakini hii Mechi na Chelsea ni nafasi yao kujibu mapigo.

Wenger amedai yeye hajali Chelsea wako nafasi gani kwenye msimamo wa Ligi bali kuona Timu yake ikisonga kwa nguvu zake zote.
Kwenye Msimamo wa Ligi, Arsenal wapo Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 10 baada ya kushinda Mechi 3, Sare 1 na Kufungwa 1 wakati Chelsea wapo Nafasi ya 17 wakiwa na Pointi 4 baada ya Kushinda Mechi 1, Sare 1 na Kufungwa 3.
Man City ndio wapo kileleni wakiwa na Pointi 15 baada ya kushinda Mechi zao zote 5.

No comments:

Post a Comment