Pages

Tuesday, September 15, 2015

NSA JOB ATOWEKA KAMBINI KWA WANA KIMANUMANU



 Nsa Jobu, Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Coastal Union na Villa Squad
MCHEZAJI wa timu ya African Sports ‘wanakimanumanu’  Nsa Job ametoweka kwenye kambi ya timu hiyo baada ya kuwepo kwa hali ya sintofahamu na uongozi wa timu hiyo
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Khatibu Enzi amesema mchezaji huyo ambaye alisajiliwa kuisaidia timu hiyo ilichopanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara msimu huu ametoweka kwenye kambi ya timu hiyo bila taarifa yoyote.
“Ni kweli Nsa Job mpaka dakika hii taarifa zake zinakwenda tofauti kwa sababu mara ya kwanza tulipata mawasiliano kwamba amepatwa na msiba lakini mpaka sasa mawasiliano yanakwenda tofauti hivyo sijapata jibu la kuweza kumjibia”, amesema Enzi.
Enzi alisema mara ya mwisho waliwasiliana naye wiki moja iliyopita akawaeleza dharura yake na wakamfanikishia, lakini kwa siku za hivi karibuni amekuwa hapatikani hivyo suala lake wameliweka pembeni kidogo wanaangalia mambo ya mechi ya kesho dhidi ya Mwadui
Pia Enzi alisema wana mkataba nae wa mwaka mmoja na klabu wanaweza kufanya marekebisho, kwasababu mikataba ipo basi watalifanyia kazi kufuatana na mkataba unasemaje.
African Sports inacheza Septemba 17 na Mwadui FC kwenye mchezo wao wa raundi ya pili huku ikiwa imechezea kichapo kwenye mechi yao ya kwanza, waliocheza na Simba kwenye uwanja wa Mkwakwani.

No comments:

Post a Comment