Pages

Saturday, September 26, 2015

NEYMAR ATHIBITISHA KUTAKWA NA KLABU YA MAN UNITED


Mshambuliaji wa Barcelona Neymar amethibitisha kuwa alikuwa na mazungumzo kuhusu kujiunga na Manchester United msimu huu lakini hakupokea ombi thabiti.
United ilihusishwa na uhamisho wa raia huyo wa Brazil, aliyefunga mabao 57 ya Barcelona mwishoni mwa dirisha la uhamisho.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amesema kuwa: ''Kulikuwa na mazungumzo lakini hakukuwepo na majadiliano ya kina''.
''Nilisikia kwamba kulikuwa na maombi lakini sikuona hata moja upande wangu''.
Naibu mwenyekiti wa kilabu ya Manchester United Ed Woodward alielekea Barcelona mwezi uliopita alipojaribu kufanikisha uhamisho wa Pedro ambaye baadaye alijiunga na Chelsea.

No comments:

Post a Comment