Pages

Wednesday, September 16, 2015

JOSE MOURINHO AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI, AZUNGUMZIA MECHI YA CHELSEA vs MACCABI TEL AVIV YA LEO


Meneja wa Chelsea Jose Mourinho akiteta jambo leo wakati akiwa kwenye mahojiano na Wahandishi wa Habari leo.
Wakati Chelsea ikikanusha kuwepo na ngumi kati ya John Terry na Diego Costa, zipo habari kuwa Meneja wao Jose Mourinho atacharuka na ‘kuwapiga shoka’ Mastaa Watatu kutoka Kikosi cha Kwanza.
Huku wakigubikwa na habari za kuwepo mzozo kati ya Kepteni wao John Terry na Straika wao Diego Costa kufuatia Timu yao kuanza vibaya Ligi Kuu England katika Miaka 29 baada ya Juzi kuchapwa 3-1 na Everton, zipo habari nzito Jose Mourinho atawatoa Wachezaji Watatu kutoka Kikosi cha Kwanza katika Mechi yao ya Jumatano ya UEFA CHAMPIONS LIGI na Maccabi Tel Aviv.
Katika Mechi 5 za Ligi walizocheza Msimu huu ili kutetea Taji lao la Ubingwa, Chelsea wamefungwa Mechi 3 na wapo Nafasi ya 17 wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Manchester City.
Mechi hiyo ya Uefa Champions ligi itachezwa kesho jumatano dhidi ya timu ya Meccabi Tel AvivJose Morinho
Cesc Fabregas, Branislav Ivanovic na Diego Costa ndio ambao wanatajwa kuwa watalivaa shoka la Mourinho kwenye Mechi yao ya kwanza ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS  LIGI Uwanjani Stamford Bridge.
Fabregas na Costa wamenyooshewa kidole kuwa uchezaji wao Msimu huu ni chini ya kiwango wakati Ivanovic amebebeshwa lawama kubwa ya kuwa uchochoro kwenye Difensi ya Chelsea ambayo Msimu uliopita ilisimama imara.
Mbali ya Mechi hii ya Jumatano, Chelsea Jumamosi wapo kwenye Dabi ya London dhidi ya Arsenal katika Mechi ya Ligi Kuu England itakayochezwa Stamford Bridge.

No comments:

Post a Comment