Pages

Thursday, September 17, 2015

HUKUMU YA MBASHA SEPTEMBA 21



 Flora <b>Mbasha</b> with her Singing Group, performing
MAHAKAMA  ya Wilaya ya Ilala imepanga Septemba 21, mwaka huu kutoa hukumu dhidi ya muimbaji wa nyimbo za injini nchini, Emmanual Mbasha (32) anayekabiliwa na mashitaka mawili ya kubaka.
Hukumu hiyo ilikuwa itolewe jana katika mahakama hiyo lakini iliahirishwa baada ya Hakimu Mkazi, Frola Mujaya anayesikiliza kesi hiyo, kuwa likizo.
Akiahirisha  kesi hiyo, Hakimu Maua Handui, alisema kuwa  kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya hukumu lakini hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, yupo likizo hivyo itakuja Septemba 21, Mwaka huu.
Katika kesi hiyo, mahakama hiyo ilifunga ushahidi wa upande wa mashitaka baada ya kusikuliza mashahidi sita.
Pia baada ya mahakama kupitia ushahidi huo, Mbasha alikutwa na kesi ya kujibu na kujitetea.
Mbasha anakabiliwa na mashtaka mawili ya kubaka binti mwenye umri wa miaka17 ambaye ni shemeji yake huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Katika shtaka la kwanza , Mbasha anadaiwa kuwa Mei 23, mwaka jana maeneo ya  Tabata Kimanga, alimbaka shemeji yake.
Pia ilidaiwa Mei 25,mwaka jana mshtakiwa huyo alimbaka shemeji yake kwenye gari aina ya Ipsum wakati akitoka kumtafuta mkewe, Flora.

                                     

No comments:

Post a Comment