Pages

Saturday, September 26, 2015

GABRIEL PAULISTA WA ARSENAL AFUNGIWA MECHI 1 NA KUTOZWA FAINI

BEKI wa Arsenal Gabriel Paulista amefungiwa na FA, Chama cha Soka England, Mechi 1 na kupigwa Faini ya Pauni 10,000 baada ya kukiri kosa la utovu wa nidhamu.
Jumamosi iliyopita, Gabriel, Mchezaji wa Brazil mwenye Miaka 24, alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu na Refa Mike Dean baada ya kufarakana na Straika wa Chelsea Diego Costa wakati Chelsea inaifunga Arsenal 2-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England huko Stamford Bridge.

Arsenal wakaikatia Rufaa Kadi Nyekundu hiyo na ikafutwa baadaa ya kushinda hiyo Rufaa.
Lakini Gabriel alikuwa akikabiliwa na Shitaka jingine kwa FA la kushindwa kutoka Uwanjani mara moja baada ya kupewa Kadi Nyekundu na kosa hilo ndio limempa Adhabu hii ya sasa.
Mbali ya Jopo la FA kuifuta Kadi Nyekundu ya Gabriel hapo Juzi, pia ilimfungia Straika wa Chelsea Diego Costa kwa kosa la kumpiga Beki wa Arsenal Laurent Koscielny bila Refa Mike Dean kuliona tukio hilo.
Mapema hii Leo, akiongea na Wanahabari kuhusu Mechi yao ya Ligi inayowakabili Jumamosi Ugenini na Newcastle, Jose Mourinho alimsema Meneja wa Arsenal Arsene Wenger bila kumtaja Jina lakini Wachambuzi wanahisi ni kutokana na sakata la Diego Costa na Gabriel.
Mourinho alisema: “Nadhani katika Nchi hii yupo Meneja mmoja tu ambae hayuko kwenye presha. Steve McClaren yuko kwenye presha, mimi niko kwenye presha, Brendan Rodgers yuko kwenye presha, Manuel Pellegrini yuko kwenye presha.”
Aliongeza: “Hatupaswi kufungwa Mechi, hatutakiwa kuwa chini ya kiwango. Yupo mmoja hayupo kwenye Listi hiyo. Ni safi kwake. Anaweza kuzungumzia Marefa kabla ya Mechi, anaweza kuzungumzia Marefa baada ya Mechi, anaweza kusukuma Watu kwenye eneo la Ufundi Uwanjani, anaweza kulia asubuhi, kulia jioni, hakuna litakalotokea.”
Mourinho alimalizia kwa kudai Meneja huyo anaweza asishinde lolote lakini akabaki kazini akiwa bado Mfalme kwa vile ana haki maalum.
Mourinho alikataa kumtaja Wenger, ambae amekuwa Meneja wa Arsenal kwa Miaka 19 na hajatwaa Ubingwa wa England tangu 2004, na kujibu: “Mnamjua ni nani!”

No comments:

Post a Comment