Pages

Tuesday, September 8, 2015

EURO 2016: ENGLAND UWANJANI LEO , ROONEY KUWEKA REKODI MPYA?

Mechi za Makundi ya EURO 2016, Kombe la Mataifa ya Ulaya, zinakamilika Leo kwa ile Raundi ya Mechi za Septemba na kubakisha Mechi 2 kwa kila Timu ambazo zitachezwa Mwezi ujao huku tayari Timu 3 zimefuzu kuingia Fainali.
Fainali za EURO 2016 zitachezwa Mwakani huko France na Raundi hii ya Mechi imezifanya England, Iceland na Czech Republic waungane na Wenyeji France kwenye Fainali.
Bado zipo nafasi 20 kukamilisha idadi ya Timu 24 kwenye Fainali ambazo huchukuliwa na Washindi 9 wa Makundi, Washindi wa Pili 9, Mshindi wa 3 Bora mmoja pamoja na Timu 4 zitakazoshinda Mechi za Mchujo zitakazoshitikisha Washindi wa 3 Wanane.

Leo England wanacheza Mechi ya kukamilisha Ratiba ya Kundi E dhidi ya Switzerland Uwanjani Wembley Jijini London na macho yote yapo kwa Kepteni wao Wayne Rooney kama ataweza kuvunja Rekodi ya Ufungaji Bora England baada Juzi kwenye Mechi na San Marino kufunga Bao moja na kumfikia Mfungaji Bora Sir Bobby Charlton mwenye Bao 49 kwa Mechi 106.

Hii Leo ataichezea England Mechi yake ya 106.


RATIBA:
Jumanne Septemba 8

21:45 Belarus vs Luxembourg
21:45 Macedonia vs Spain
21:45 Slovakia vs Ukraine
21:45 England vs Switzerland
21:45 Slovenia vs Estonia
21:45 Lithuania vs San Marino
21:45 Liechtenstein vs Russia
21:45 Sweden vs Austria
21:45 Moldova vs Montenegro

No comments:

Post a Comment