Pages

Thursday, September 24, 2015

DOKTA EVA CARNEIRO ATIMKA CHELSEA, MBIONI KUIBURUZA KWA PILATO KWA UBAGUZI WA JOSE MOURINHO


Zimeibuka taarifa kuwa Daktari wa Chelsea Mwanamama Eva Carneiro ameacha kazi Klabuni hapo na yupo mbioni kuifungulia Mashitaka.
Dokta huyo aliondolewa kuihudumia Timu ya Kwanza ya Chelsea baada ya Mechi ambayo Chelsea walitoka 2-2 na Swansea hapo Agosti 8.
Katika Mechi hiyo,Dokta Carneiro na Tabibu wa Viungo Jon Fearn waliingia Uwanjani kumtibu Eden Hazard kwenye Dakika za Majeruhi wakati Chelsea ipo 2-2 na Swansea City huku wakiwa Mtu 10 baada ya mapema Kipa wao Thibaut Courtois kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Kitendo hicho kilimkera Mourinho kwani Mchezaji akihudumiwa na Madokta basi huwajibika kutoka nje ya Uwanja na husubiri amri ya Refa kuingia tena huku Gemu ikiendelea na hilo liliiacha Chelsea iwe Mtu 9 kwa Dakika kadhaa.
Mourinho alimponda Dokta huyo na kumsema hajui mchezo unakwendaje.
Tukio hilo lilizua hisia kali na Juzi Mdau mmoja kuamua kulalamika kwa FA, Chama cha Soka England, kuwa Mourinho alimfokea Dokta Eva Caerneiro kwa kutumia lugha chafu na sasa FA imeamua kuchunguza tukio hilo.
Imeripotiwa kuwa Dokta Eva Carneiro alitakiwa arudi kazini tangu Ijumaa iliyopita lakini hakufanya hivyo na sasa yuko mbioni kusaka Sheria katika mamlaka husika.

No comments:

Post a Comment